FIFA YAIBEBA TANZANIA VIWANGO VYA SOKA DUNIANI NA AFRIKA

Wakati Timu ya Taifa ya Tanzania Ikisubiri kucheza mchezo wa mwisho wa kuwania nafasi ya tatu katika mashindano ya COSAFA Challenge Cup Shirikisho la soka Duniani limeinyanyua Tanzania kwenye Viwango ubora wa soka Duniani kwa mwezi wa Sita ikipanda kwa nafasi 25 katika viwango hivyo vinavyotolewa kila mwezi.

Mabingwa wa Dunia ambao juzi walitawazwa kuwa mabingwa wa kombe la mabara Ujerumani ndiyo vinara wa soka duniani katika orodha hiyo huku Tanzania ikipanda mpaka nafasi ya 114 duniani na nafasi ya 26 kwa Afrika ikiipiku Burundi ambayo ni ya 31 Afrika na 121 Duniani, Burundi ikikamata 33 na 127 Duniani.

Uganda Ndiyo inayoongoza kwa Afrika Mashariki ikikamata nafasi ya 13 Afrika na 74 kwa duniani. Kenya Wanafatia wakiwa katika nafasi ya 14 afrika na 84 duniani.

Tanzania Itacheza na Rwanda siku chache zijazo katika kuwania nafasi ya kushiriki fainali ya kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa Ndani mchezo utakaopigwa Jijini Mwanza.

Takwimu za ubora ni kama ifuatavyo:

Kumi ubora viwango vya Soka Duniani
  1. Ujerumani  
  2. Brazil
  3. Argentina
  4. Ureno
  5. Switzerland
  6. Poland
  7. Chile
  8. Colombia
  9. Ufaransa
  10. Ubeligiji 
Kumi bora viwango vya Soka Afrika, duniani kwenye mabano
  1. Misri nafasi   (23)
  2. Senegal (27)
  3.  Congo DRC (28)
  4.  Cameroon (36)
  5.  Nigeria (39)
  6.  Burkina Faso(44)
  7.  Algeria (48)
  8.  Ivory Coast (56)
  9.  Mali (59)
  10.  Morocco (60)


No comments

Powered by Blogger.