ARSENAL NA LEICESTER CITY KUFUNGUA LIGI KUU ENGLAND MSIMU UJAO SIKU YA IJUMAA

Arsenal v Leicester City on Friday, August 11, will kick off the 2017/18 Premier League season
Marekebisho ya mechi kadhaa za ligi kuu nchini Engaland yametolewa leo kwa Baadhi ya mechi kubadilishiwa tarehe na siku kutokana na Haki ya matangazo ya televisheni na hii kuathiri pia hata mechi za Ufunguzi wa ligi hiyo ambapo sasa Ligi hiyo imerudishwa nyuma kwa siku moja na itaanza siku ya Ijumaa ya tarehe 11 baada ya jumamosi ya Tarehe 12 Agosti 2017.

Pambano baina ya Arsenal na mabingwa wa zamani wa Ligi hiyo Leicester City zitakutana katika mechi ya ufunguzi kwenye dimba la Emirates siku hiyo ya Ijumaa.

Mechi baina ya watford dhidi ya Liverpool na ile ya Brighton dhidi ya Manchester City zitachezwa Jumamosi ya Tarehe 12 huku Manchester United dhidi ya West Ham ikipigwa Jumapili Sambamba na ile ya Tottenham dhidi ya Newcastle ugenini.


No comments

Powered by Blogger.