YANGA WANYOOSHA MIKONO JUU, WATANGAZA KUMSHINDWA NIYONZIMA.

Kile kitendawili cha kiungo mahiri wa Yanga, raia wa Rwanda Haruna Niyonzima ambacho kimekua kikisumbua vichwa vya wapendasoka wengi hapa nchini hatimaye ni kama kimeteguliwa baada ya klabu yake ya Yanga kutangaza kutoendelea kuwa nae msimu ujao baada ya kushindwa kufikia makubaliano ya kusaini mkataba mpya.

Mkataba wa Niyonzima na Yanga utamalizika mwishoni mwa mwezi huu na wapendasoka.com inafahamu kwamba mazungumzo yalikua yakiendelea kati yao huku Simba nao wakiwa wameweka donge nono mezani kwa ajili ya kumnasa nahodha huyo msaidizi wa Yanga.

Taarifa hiyo ni ishara kwamba sasa Niyonzima atavaa jezi za rangi nyekundu na nyeupe msimu ujao kwa dau linalotajwa kuwa ni zaidi ya shilingi milioni 100 za kitanzania.

No comments

Powered by Blogger.