UJERUMANI WANG'ARA MBELE YA AUSTRALIA KOMBE LA MABARA.

Michuano ya kombe la mabara imeendelea tena jana usiku kwa mchezo wa mmoja wa kundi B uliowakutanisha Mabingwa wa Kombe la Dunia Ujerumani dhidi ya timu ya Australia ambapo
Ujerumani waliibuka vinara katika mchezo huo kwa kuwafunga Austria mabao 3-2.

Magoli ya Ujerumani yalifungwa na Lars Stindl dakika ya 5, Julian Draxler kwa mkwaju wa penati dakika ya 45 na Leon Goretzka huku magoli ya Australia yakiwekwa kimiani na Tom Rogic na Tom Jurick

Michuano hiyo inatarajiwa kuendelea tena Kesho baada ya mapumziko mafupi leo.

No comments

Powered by Blogger.