UCHAGUZI TFF SASA RUKSA:BMT
Katika barua yake iliyoandikwa Juni 19, mwaka huu na kusainiwa na Katibu Mkuu wa BMT, Mohammed Kiganja, Baraza hilo limesema: “Uchaguzi huu usivuruge amani iliyopo nchini. Wagombea wakumbuke kuwa kuna maisha baada ya uchaguzi.”
Pia Baraza limeiagiza TFF kuwaelimisha wote na kuwasisitiza kuzipitia sheria za Baraza la Michezo, Kanuni za Baraza na kanuni za Usajili, hususani kanuni ya 8 (1) na (2).
Kanuni hiyo ya 8 (1) na (2), inaagiza kuwa endapo wagombea wote watakaoshinda nafasi wanazowania kwa sasa ndani ya TFF, hawana budi kuachia nafasi mojawapo katika uongozi wa mpira kwa miguu katika ngazi ya wilaya au mkoa aliyoshinda awali.
Viongozi watakaopatikana wanatakiwa kula kiapo cha utii, na kujaza fomu Namba 5 ya BMT ya utekelezaji majukumu yao kwa mujibu wa Kanuni ya 8 (4)
Kadhalika, mara baada ya uchaguzi, Baraza limeagiza kuhusisha baadhi ya vifungu vya sheria ya Baraza ili viendane na katiba za TFF na wadau pamoja na kanuni zao.
Uchaguzi huo unategemewa kufanyika Dodoma Tanzania tarehe 12/8/2017

No comments