UCHAGUZI SASA TFF KUFANYIKA AGOSTI
Kamati ya Uchaguzi ya
Shirikisho la Mpira wa Tanzania (TFF), imetangaza Uchaguzi Mkuu wa shirikisho
hilo utakafanyika Agosti 12, mwaka huu mjini Dodoma.
“Napenda kuwatangazia
wadau wote wa mpira wa miguu kuwa mnakaribishwa kugombea nafasi zilizo
orodheshwa hapo chini kwa kuchukua fomu Ofisi za TFF Karume Ilala na pia
unaweza kuzipata katika tovuti ya TFF: www.tff.or.tz,” amesema Kuuli.
Akitangaza tarehe hiyo
mbele ya wanahabari, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa TFF, Wakili Revocatus
Kuuli, amesema kwamba kamati yake haitakuwa na huruma kwa ishara yoyote ya
rushwa katika kipindi chote cha uchaguzi.
Wakili Kuuli amesema
kamati yake itandesha uchaguzi huo kwa Uhuru na Haki na kuzingatia taratibu,
kanuni na sheria zote zilizopo.
Kuuli, amesema Kamati
yake itafanya kazi na Taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na jeshi la Polisi kuhakikisha uchaguzi huo
hautakuwa na vitendo vya rushwa.
“Tunawatahadharisha
wagombea woye kukaa mbali na vitendo vya rushwa…, kamati yetu haitakubali
vitendo hivyo na tutafanya kazi na mamlaka za Serikali kuhakikisha yeyote
atakayehusika na vitendo hivi anachukuliwa hatua, Takukuru wataufuatilia kwa
karibu uchaguzi huu,” alisema Kuuli.
Akizungumzia mchakato
mzima, Kuuli anasema, mchakato wa kuchukua fomu na kuzirejesha ni Juni 16 mpaka
20, mwaka huu na kikao cha mchujo wa awali kwa wagombea kitafanyika Juni 21
mkapa Juni 23.
Juni 24 na 25, mwaka
huu, kamati itafanya kazi ya kuchapisha na kubandika kwenye mbao za matangazo
majina ya wagombea wakati Juni 26-28 zitakuwa siku za kupokea na kuweka
mapingamizi kwa wagombea na Juni 29 mpaka Julai Mosi itakuwa kipindi cha
kupitia mapingamizi yote na kufanya usaili.
Kwa mujibu wa Kuuli,
Julai 2-3 kitakuwa kipindi cha kuchapisha na kubandika matokeo ya usaili, Julai
4-7 na kipindi cha Sektretarieti kuwasilisha masuala ya Kimaadili kwenye Kamati
ya maadili, Julai 7-11 ni kipindi cha kusikiliza na kutolea maamuzi masuala ya
kimaadili.
Julai 15-17 kitakuwa
kipindi cha kukataa Rufaa kwa maamuzi ya masuala ya kimaadili kwenye
kamati ya rufaa ya Maadili ya TFF, Julai 18-22 itakuwa siku ya kusikiliza rufaa
za maadili na Julai 23 mpaka Julai 25 itakuwa siku ya kutoa maamuzi ya Rufaa,
Julai 26-28 kitakuwa kipindi cha kukata rufaa dhidi ya kamati ya Uchaguzi
kwenye Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF, rufaa hizo zitasikilizwa Julai 29
mpaka Agosti 2.
Wagombea watajulishwa
matokeo ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF na Agosti 5-6 itakuwa siku ya kuchapisha
majina ya wagombea watakaoingia kwenye Uchaguzi huo na kampeni kwa wagombea
zitaanza Agosti 7 mpaka 11 na siku inayofuata yaani Agosti 12 itakuwa siku ya
uchaguzi wa viongozi wa TFF.
Nafasi zinazogombewa
ni Rais wa TFF, Makamu wa Rais pamoja na nafasi 13 za wajumbe TFF
wanaowakilisha kanda 13 za Kagera na Geita;
Mara na Mwanza;
Shinyanga na Simiyu;
Arusha na Manyara;
Kigoma na Tabora;
Katavi na Rukwa;
Mbeya na Iringa;
Njombe na Ruvuma;
Lindi na Mtwara;
Dodoma na Singida;
Pwani na Morogoro;
Kilimanjaro na Tanga
na
Dar es Salaam ambayo
ni kanda pekee.
Sifa za wagombea
GHARAMA ZA KUCHULIA
FOMU.
1. Rais TSHS 500,000/=
2. Makamu wa Rais TSHS 300,000/=
3. Wajumbe wa kamaki ya utendaji TSHS 200,000/-
SIFA ZA WAGOMBEA.
- 1.
Awe raia wa Tanzania.
- 2.
Awe na kiwango cha elimu kisichopungua kidato cha nne (Cheti cha
Elimu ya Sekondari).
- 3.
Awe na uzoefu wa uendeshaji Mpira wa Miguu uliothibitishwa wa angalau
miaka mitano.
- 4.
Asiwe na hatia yoyote ya kosa la jinai na asiwe amewahi kuhukumiwa
kifungo kisicho na mbadala wa faini.
- 5.
Awe na umri angalau miaka 25.
- 6.
Awe amewahi kuwa ama Mchezaji Mpira wa Miguu, Kocha, Mwamuzi. Au
kushiriki katika uendeshaji wa Mpira wa Miguu angalau katika ngazi ya
Mkoa au ngazi ya daraja la kwanza.
- 7.
Awe muadilifu na muaminifu mwenye uwezo wa utendaji katika utekelezaji na
utimizaji wa majukumu na malengo ya TFF.
- 8.
anayegombea nafasi ya Rais au makamu wa Rais awe na kiwango cha elimu
kisichopungua shahada moja, mwenye utu na uwezo wa kuiwakilisha TFF ndani
na nje ya nchi.
Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni tarehe 16-20/06/2017 saa
kumi (10:00) jioni.
MCHAKATO MZIMA WA
UCHAGUZI NI KAMA UFUATAVYO:
1
|
14-15/06/2017
|
Kutangaza mchakato
wa Uchaguzi wa TFF nafasi zinazogombewa na kubandika kwenye mbao za
matangazo
|
Mwenyekiti wa kamati
ya Uchaguzi TFF
|
10.7
|
2
|
2
|
16-20/06/2017
|
Kuanza kuchukua fomu
za kugombea. Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu za kuomba uongozi.
|
Wagombea wote
|
10.8
|
5
|
3
|
21-23/06/2017
|
Kikao cha mchujo wa
awali wa wagombea na Kuandika barua za Kuwajulisha wagombea juu ya mchujo wa
awali
|
Kamati ya Uchaguzi
TFF
|
11.1
|
3
|
4
|
24-25/06/2017
|
Kuchapisha na
kubandika kwenye mbao za matangazo orodha ya awali ya wagombea
|
Kamati ya Uchaguzi
TFF
|
11.2
|
2
|
5
|
26-28/06/2017
|
Kipindi cha kupokea
na kuweka pingamizi kwa wagombea
|
Wagombea
|
11.3 - 4
|
3
|
6
|
29/6-1/7/2017
|
Kupitia pingamizi
zote na kufanya usaili wa wagombea
|
Kamati ya uchaguzi
na Wagombea
|
11.7
|
3
|
7
|
02-03/07/2017
|
Kutangaza na
kubandika kwenye mbao za matangazo Matokeo ya awali ya usaili
|
Kamati ya Uchaguzi
TFF
|
11.8
|
2
|
8
|
04-06/07/2017
|
Sekretariati
kuwasilisha masuala ya kimaadili kwenye kamati ya Maadili
|
Kamati ya maadili ya
TFF
|
11.10
|
3
|
9
|
07-11/07/2017
|
Kipindi cha Kupokea
na kusikiliza na kutolea Maamuzi masuala ya maadili
|
Kamati ya Maadili ya
TFF
|
11.10
|
5
|
10
|
12-14/07/2017
|
Kutangaza matokeo ya
maamuzi ya kamati ya Maadili
|
Kamati ya Maadili ya
TFF
|
11.10
|
3
|
11
|
15-17/07/2017
|
Kipindi cha
kukata Rufaa kwa Maamuzi ya Masuala ya Kimaadili kwenye kamati ya rufaa ya
Maadili ya TFF
|
Wagombea
|
11.11
|
3
|
12
|
18-22/07/2017
|
Kusikiliza rufaa za
kimaadili
|
Kamati ya rufaa ya
maadili ya TFF na Wagombea.
|
11.12
|
5
|
13
|
23-25/07/2017
|
Kutoa maamuzi ya
Rufaa
|
Kamati ya rufaa ya
maadili ya TFF.
|
11.12
|
3
|
14
|
26-28/07/2017
|
Kipindi cha Kukata
Rufaa Dhidi ya Kamati ya Uchaguzi kwenye kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF
|
Wagombea na Katibu
Mkuu TFF.
|
13.1
|
3
|
15
|
29/7-2/8/2017
|
Rufaa kusikilizwa na
kamati ya rufaa ya Uchaguzi ya TFF
|
Kamati ya Rufaa ya
Uchaguzi ya TFF na Wagombea
|
13.2
|
5
|
16
|
03-04/08/2017
|
Wagombea na kamati
ya uchaguzi kujulishwa maamuzi ya Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF
|
Kamati ya Rufaa ya
Uchaguzi ya TFF
|
13.3-4
|
2
|
17
|
05-06/08/2017
|
Kuchapisha orodha ya
Mwisho ya Wagombea na kutangazwa na kubandikwa kwenye mbao za matangazo
|
Kamati ya uchaguzi
TFF.
|
14.1
|
2
|
18
|
07-11/08/2017
|
Kipindi cha kampeni
kwa wagombea
|
Wagombea
|
14.3
|
5
|
19
|
12/08/2017
|
Uchaguzi Mkuu wa TFF
|
Wagombea
Wajumbe na Kamati ya
Uchaguzi TFF
|
14.4
|
1
|
No comments