TAIFA STARS YATAKATA MICHUANO YA COSAFA.
Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars leo imefanikiwa kusonga mbele katika hatua ya robo fainali baada ya kuibuka kinara wa kundi. A
Stars imevuna pointi 5 katika michezo mitatu baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Mauritius katika mchezo uliopigwa jioni ya leo.
Bao la Stars katika mchezo huo limefungwa na Saimon Msuva mnamo dakika ya 67, dakika moja baada ya Perticots kuiandikia Mauritius bao la kuongoza.
Katika mchezo mchezo mwingine, Angola wametoka sare ya bila kufungana na Malawi, matokeo ambayo yamewafanya Angola kufikisha pionti 5 sawa na Tanzania lakini Tanzania inasonga mbele kwa tofauti nzuri ya mabao.
Stars sasa watakua na kibarua cha kuvaana na wenyeji Afrika Kusini katika mchezo wa robo fainali Jumapili ya Julai 2

No comments