GOMIS APOKELEWA KWA SHANGWE GALATASARAY


Mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa Bafetimbi Gomis amejiunga na Galatasaray ya Uturuki akitokea Swansea.

Jijini Instanbul Gomis alilakiwa na mamia ya mashabiki wa Galatasaray ikiwa ni wiki moja tu tangu Methiew Valbuena alipojiunga na klabu hiyo pia akitokea Ufaransa.

Msimu uliopita alicheza Marseille kwa mkopo akifunga magoli 21 katika mechi 31 za Ligi kuu Ufaransa.

Gomis mwenye miaka 32 Hakuwa na msimu mzuri akiwa na Swansea tangu alipojiunga nayo mwaka 2014 akitokea Olympic Lyon akifunga mabao 17 katika mechi 71 na anajiunga na Galatasaray kwa ada ya uhamisho paundi milioni 5.

No comments

Powered by Blogger.