NYAMLANI AJITOA KUWANIA URAIS TFF

Makamu wa Rais wa zamani wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Athumani Nyamlani amejitoa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania urais wa shirikisho hilo unaotarajiwa kufanyika Agosti 12, mwaka huu.


Nyamlani aliwasilisha barua TFF leo Jumapili Juni 25, mwaka huu ikiwa ni siku moja tu tangu Kamati ya Uchaguzi ipitishe jina lake kuwa miongoni mwa wagombea 10 wanaowania nafasi hiyo ya urais. Sababu aliyoeleza ni masuala binafsi.


Kwa msingi huo, wagombea wanaobaki kwenye kinyang’anyiro na kuhitajika kufika kwenye usaili kuanzia Juni 29, mwaka huu ni tisa wakiongozwa na Rais wa sasa, Jamal Malinzi anayetetea nafasi.


Mbali ya Malinzi wengine wanaowania nafasi hiyo ni Imani Madega, Wallace Karia, Fredrick Masolwa, Fredrick Mwakalebela, John Kijumbe, Shija Richard, Ally Mayay na Emmanuel Kimbe.


Waliojitokeza kuwania Makamu wa Rais na kurejesha fomu wako Mulamu Ng’hambi, Michael Wambura, Geofrey Nyange, Mtemi Ramadhani, Robert Selasela na Stephen Mwakibolwa.


Mbali ya nafasi za urais na makamu rais, Abdallah Mussa - aliyekuwa akiwania nafasi ya kugombea ujumbe wa Kamati ya Utendaji TFF kutoka Kanda Na. 1 (Mikoa ya Kagera na Geita) aliondolewa kwa sababu ya kutoambatanisha kivuli cha cheti ya elimu ya sekondari.


Hivyo wagombea wa nafasi za Wajumbe wa Kamati ya Utendaji kwa kufuata Kanda 13 ni kama ifuatavyo:


Kanda Na. 1 Mikoa ya Kagera na Geita;

Soloum ChamaKaliro SamsonLeopold Mukebezi

Kanda Na. 2 Mikoa ya Mara na Mwanza;

Vedastus LufanoEphraim MajingeSamwel DanielAaron Nyanda


Kanda Na. 3 Mikoa ya Shinyanga na Simiyu;

Benista RugoraMbasha MatutuStanslaus Nyongo


Kanda Na. 4 Mikoa ya Arusha na Manyara;

Omari WaliiSarah ChaoPeter Temu


Kanda Na. 5 Mikoa ya Kigoma na Tabora;

John KadutuIssa BukukuAbubakar ZeboFrancis Michael


Kanda Na. 6 Mikoa ya Katavi na Rukwa;

Kenneth PesambiliBaraka Mazengo


Kanda Na. 7 Mikoa ya Mbeya, Songwe na Iringa;

Elias MwanjalaCyprian KuyavaErick AmbakisyeAbousuphyan Silliah


Kanda Na. 8 Mikoa ya Njombe na Ruvuma;

James MhagamaGolden SangaVicent MajiliYono Kevela


Kanda Na. 9 Lindi na Mtwara;

Athuman KambiDunstan Mkundi


Kanda Na. 10 Mikoa ya Dodoma na Singida;

Hussein MwambaMohamed AdenMusa SimaStewart Masima Ally SuruGeorge Benedict


Kanda Na. 11 Mikoa ya Pwani na Morogoro;

Charles MwakambayaGabriel MakwaweFrancis NdulaneHassan Othman ‘Hassanol’


Kanda ya 12. Mikoa ya Kilimanjaro na Tanga

Khalid MohamedGoodluck MoshiThabit Kandoro


Kanda Na. 13 Mkoa wa Dar es Salaam

Emmanuel AsheryAyoub NyenziSaleh AlawiShaffih DaudaAbdul SaukoPeter MhinziAlly KamtandeSaid TullyMussa KisokyLameck NyambayaRamadhani NassibAziz KhalfanJamhuri KihweloSaad KawembaBakari Malima

No comments

Powered by Blogger.