KICHUYA AING'ARISHA TAIFA STARS WAKIANZA KWA USHINDI MICHUANO YA COSAFA.

Pazia la michuano ya soka kwa nchi za ukanda wa kusini mwa Africa COSAFA limefunguliwa leo kwa mchezo kati ya Tanzania ambao ni waalikwa dhidi ya Malawi.

Taifa Stars imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo huo huku mabao yote yakifungwa katika kipindi cha kwanza na Shiza Kichuya.

Kichuya alifunga bao la kwanza katika dakika ya 13 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Saimon Msuva.

Kichuya alirudi tena 'kambani' katika dakika ya 18 baada ya kuichambua ngome ya Malawi na kupiga shuti hafifu lililomwacha golikipa wa Malawi na kutinga wavuni.

Mpaka dakika 45 zinamalizika, Tanzania ilikua mbele kwa mabao 2-0.

Kipindi cha pili kilikua cha piga nikupige, Malawi wakijitahidi kusawazisha, lakini ukuta wa Tanzania ukiongozwa na Salim Mbonde ulisimama imara.

Stars walifanya mabadiliko kwa kuwatoa Elius Maguli, Shiza Kichuya na Saimon Msuva na nafasi zao kuchukuliwa na Ramadhan Kessy, Nurdin Chona na Mbaraka Yusuf ambao waliubadilisha mchezo kwa kiasi kikubwa.

Mpaka mchezo unamalizika Tanzania iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Taifa Stars itarudi tena dimbani tarehe 27 kukipiga dhidi ya Angola.

No comments

Powered by Blogger.