MAN UNITED YAANZA USAJILI : BONGE LA BEKI TOKA SWEDEN ASAINI MIAKA MINNE


Victor Lindelof
Moja kati ya mabeki bora kabisa wa kikosi cha timu ya taifa ya Sweden amesaini jana kujiunga na Mourinho's Revolution.

Paundi milioni 31 zimetolewa na Manchester United kumpata kijana huyu mwenye miaka 22 tu akitokea Benfica ya Ureno beki anayetajwa kuweza kucheza nafasi yoyote katika nafsi nne za upande wa Ulinzi.

Victor amesaini kuichezea Manchester United kwa mkataba wa miaka minne kukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mmoja.

Moja kati ya Eneo lililokua likimsumbua kocha Jose Mourinho ni majeruhi upande wa safu yake ya Ulinzi na sasa kwa kumsajili Victor ni dhahiri ameanza kutibu ugonjwa huo.

Kama Ilivyokua msimu uliopita United walianza kwa kumsajili beki Eric Bailly ndivyo msimu huu wa usajili wameanza pia na beki Victor Lindelof.

No comments

Powered by Blogger.