LICHA YA KULIPIWA KILA KITU, TBS YAPIGA 'STOP' NYASI ZA UWANJA WA SIMBA NA HIZI NDIZO SABABU
Zile ndoto za mashabiki
wa Simba kuweza kupata uwanja wao zimeendelea kuota mbawa baada ya kushindwa
kupatikana kwa Nyasi bandia za klabu hiyo ambazo zilikua zimekwama muda mrefu
bandarini kufuatia kucheleweshwa kulipiwa Ushuru kwa mamlaka ya mapato Tanzania
TRA.
Tayari Simba walishalipa
fedha zilizokuwa zikitakiwa na TRA pamoja na gaharama za utunzaji wa nyasi hizo
lakini wakiwa wanajiandaa kwaajili ya kuzipeleka Bunju katika uwanja husika
Shirika la Viwango Nchini Tanzania TBS liliibuka na kudai risiti halisi za
nyasi hizo na Simba kushindwa kuzitoa kwani walikua na Vivuli tu vya risiti
hizo na hata zilipofatiliwa Nchini China bado mpaka sasa imeshindikana
kupatikana.
Taarifa ambazo www.wapendasoka.com Imezipata zinaeleza kwamba kwa kukosa huko kupata risiti halisi ya nyasi hizo Simba wanatakiwa kulipa faini ya milioni 37 Swala ambalo halijapatiwa ufumbuzi ndani ya klabu hiyo na huenda swala hilo likachukua muda mwingi zaidi mpaka TBS watakaporuhusu kuchukuliwa nyasi hizo.
Aidha hati ya Ukaguzi wa nyasi hizo ulishafanyika na Simba wana kivuli cha ukaguzi huo ambacho ndicho kilichopelekea kusafirishwa kwa nyasi hizo.
WITO WETU:
Kama Wapenda Soka
Tungependa kuona swala hili linamalizika kwa maendeleo ya mpira wetu Tanzania
ni vyema Viongozi wa Simba wakamshirikisha Waziri wa habari Sanaa utamaduni na
Michezo ili kuweza kupata ufumbuzi wa jambo hili.
No comments