HIKI HAPA KIKOSI CHA STARS KITAKACHOSHIRIKI COSAFA
Kocha Mkuu wa timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Salum
Shabani Mayanga, leo Jumatano Juni 14, 2017 ametangaza majina ya wachezaji 22
watakaounda kikosi kinachokwenda kushindana kuwania Kombe la Castle Cosafa
nchini Afrika Kusini.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti,
inatarajiwa kuanza kambi rasmi Jumapili Juni 18, mwaka huu. Kambi hiyo itakuwa
kwenye Hoteli ya Urban Rose, iliyoko Mtaa wa Jamhuri katikati ya jiji la Dar es
Salaam.
Taifa Stars inajiandaa na michuano ya Cosafa inayotarajiwa
kuanza Juni 25, mwaka huu. Michuano hiyo, inaandaliwa na Baraza la Mpira wa
Miguu la nchi za Kusini mwa Afrika ambako Tanzania - mwanachama wa Cecafa,
imepata mwaliko kushiriki.
Tanzania imepangwa kundi A ambako wapinzani wake ni
Mauritius, Malawi na Angola wakati Kundi B ni Msumbiji, Shelisheli, Madagascar
na Zimbabwe. Timu za Botswana, Zambia na Afrika Kusini kadhalika Namibia,
Lesotho na Swaziland zitakuwa na mechi maalumu (play off) ili kuingia robo
fainali.
Kwa mujibu wa Mayanga kikosi hiko kinaundwa na
MAKIPA
Aishi
Salum Manula (Azam FC), Benno David
Kakolanya (Young Africans SC) na Said
Mohammed Said (Mtibwa Sugar FC).
WALINZI
Shomari
Salum Kapomb (Azam FC) Hassan Ramadhan
‘Kessy’ (Young Africans SC) Gadiel Michael (Azam FC) na Amim Abdulkarim (Toto
Africans FC).Erasto Nyoni (Azam FC),
Salim Hassan Abdallah (Mtibwa Sugar), Abdi Banda (Simba SC) na Nurdin Chona
(Tanzania Prisons)
VIUNGO
Himid
Mao (Azam FC) na Salmin Hoza wa Mbao FC.Mzamiru Yassin Selembe (Simba), Simon
Happygod Msuva (Young Africans SC), Raphael Daudi (Mbeya City) na Shizza
Ramadhani Kichuya (Simba SC).
WASHAMBULIAJI
Thomas
Emmanuel Ulimwengu (AFC Eskilstuna – Sweden), Mbaraka Abeid Yusufu (Kagera
Sugar), Stamili Mbonde, Elius Maguli (Dhofar SC) na Shabani Idd Chilunda (Azam
FC).
No comments