EPL NI NGUMU KUTOBOA BALLON D'OR: VICTOR WANYAMA

 
Safari ya kuelekea mafanikio katika kabumbu haikuwa rahisi, ilimbidi asote Sana Huko Sweden, Belgium kabla ya kuibukia Celtic ya Uskochi.

Mechi kati ya Barcelona na Celtic Ya November 7, 2012 Itakuwa ni mechi ya kukumbukwa daima katika maisha ya soka kwa Victor Wanyama. Ni mechi ambayo Wanyama alikichafua balaa pale kati lakini kubwa zaidi akafunga moja ya magoli muhimu na kuiweka Celtic katika nafasi ya kufuzu Hatua ya 16 bora kwenye michuano ya Klabu Bingwa Ulaya.

Southampton Wakamuona na wakamleta katika Ligi kuu England, akawa na msimu mzuri na Totenham wakamsogeza North London akajiunga na Totenham na amekuwa na msimu mzuri sana Totenham huku akiisadia yimu yake kukalia kiti cha nafasi ya pili katika ligi kuu England.

Victor Wanyama sasa yupo Tanzania kwa ajili ya mapumziko kabla ya kuanza msimu mpya wa Ligi Kuu England, Akiongea na Kipindi Cha FNL Kinachorushwa kupitia channel ya East Africa TV, Wanyama alipoulizwa kuhusu Wachezaji wa EPL Kushinda Tuzo ya mwanasoka bora wa Dunia alikuwa na haya ya kusema "EPL ni ngumu, ni ngumu mno kuliko ligi zingine kama La Liga, Bundesliga au hata Serie A, Ugumu wa EPL ndiyo unasababisha mchezaji mmoja kuwa juu zaidi ya wengine tofauti na ligi zingine ambazo unakuta wachezaji wachache wako juu sana kimafanikio tofauti na wenzao"

Wanyama aliendelea kwa kusema "Mchezaji wa EPL akihamia ligi nyingne ni rahisi sana kwake kufanikiwa kuliko akiwa EPL sababu ya ushindani na ugumu uliopo katika ligi hiyo"

Alipoulizwa kuhusu Ronaldo na Messi Wanyama alikuwa na haya "Kwanza ni dhambi kuwalinganisha hawa watu wawili, kwani wao wapo katika dunia ya kwao peke yao, kila mmoja anauzuri wake kumzidi mwingine hivyo ni ngumu sana kuwalinganisha hawa wawili, lakini kama ukiniuliza mimi nitachagua Ronaldo sababu mimi ni shabiki wa Ronaldo"

Na vile vile Wanyama walipoulizwa kuhusu Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga KRC Genk ya huko Belgium, Wanyama alisema "Sijawahi kukutana ana kwa ana na Samatta, lakini nimekuwa nikimsikia na kumfatilia, alikuwa na msimu mzuri sana na KRC Genk katika msimu uliyoisha"

Wanyama aliendelea kwa kusema "kama Samatta akiendelea na kuongeza juhudi katika msimu ujao, basi timu kutoka German, England au hata Ufaransa na Spain zitapiga hodi kutaka saini yake, kwani yeye (Samatta) ni mchezaji mzuri"

Wanayama alimalizia kwa kusema kuwa yeye anaamini yupo kwenye timu sahihi na wala hana mpango wa kuondoka Spurs, kwani kwake yeye Spurs sasa ni timu kubwa na imebakisha kitu kidogo sana kuanza kubeba vikombe, pia Wanyama anaamini kuwa furaha kubwa kwake ni kubeba vikombe na timu aliyshiriki kujenga mafanikio kuliko kukimbilia timu kubwa ambazo zimekuwa na kawaida ya kubeba vikombe.

Hayo ni ya Victor Wanyama vipi kwako unasemaje, maoni yako ni muhimu hapa chini.

No comments

Powered by Blogger.