SIMBA YAISHITAKI TFF KWA FIFA
Wekundu wa Msimbazi Simba Sports Club imeamua kuliburuza Shirikisho la mpira wa
miguu Tanzania (TFF) hadi katika mahakama ya usuluhishi ya FIFA (CAS) kwa ajili
ya kupata haki yake kufuatia suala la kupokwa pointi tatu kufuatia Kagera Sugar
kumchezesha mchezaji mwenye kadi tatu za njano.
Rais wa klabu hiyo Evans Aveva alisema kuwa sababu
tatu zilizotolewa na Kamati ya Katiba Sheria na Hadhi za Wachezaji hazikuwa na
mashiko kwani suala la mchezaji kucheza akiwa na kadi tatu ni kosa kwa mujibu
wa kanuni.
Rais Aveva amewaambia waandishi wa habari makao
makuu ya klabu hiyo kuwa timu yake ya Simba imekuwa ikionewa na TFF kutokana na
maamuzi mbalimbali yanayotolewa ndiyo maana wakaamua kupeleka malalamiko yao
FIFA.
Simba ina subiri kupewa barua na (TFF) inayo onyesha kupokwa pointi hizo ili kuweza kupeleka malalamiko yao (CAS) kwa ajili ya kupata alama hizo ambazo wanasema ni halali kwao.

No comments