SIMBA YAENDELEZA USHINDI,STAND UNITED YATULIZWA DAR


Wekundu wa Msimbazi Simba wamepania kumaliza msimu huu wa ligi kuu ya soka Tanzania bara bila kupoteza mechi yoyote baada ya kuwafunga Stand United bao 2-1.

Bao la sekunde ya 26 baada ya mpira kuanza likifungwa na Selemani Cassim wa Stand United liliwarudisha Simba mchezo na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha dakika ya 24 likifungwa na mshambuliaji Juma Luizio kisha akafunga bao la pili dakila 10 baadae.

Matokeo hayo ndiyo yaliyodumu mpaka mwisho wa mchezo na kuwapa Simba ushindi muhimu ambao unawarudisha kileleni mwa Msimamo wa ligi hiyo inayoelekea ukingoni.


No comments

Powered by Blogger.