AZAM FC YAIADHIBU TOTO AFRICANS BILA HURUMA


Wana Lambalamba Azam FC wameweza kuibuka na ushindi mnono wa bao 2-0 dhidi ya timu isiyotabirika ya Toto Africans ya Mwanza katika mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara.

Mchezo huo uliopigwa usiku katika dimba la Chamazi jijini Dar ea Salaam ulikua mkali huku makosa machache yakiigharimu Toto Africans na kuweza kupoteza mchezo huo.

Shabani Idd aliipatia Azam FC bao la kwanza kwa kichwa akiunganisha krosi ya Bruce Kangwa kisha Ramadhani Singano akaifungia Azam FC bao la pili akiunganisha krosi ya Shomari Kapombe.

Toto Afrika ikiwa katika balaa la kushuka daraja sasa watakua wakiombea wapate uahindi katika mechi zao 2 zilizobaki dhidi ya Mtibwa Sugar na Yanga.

No comments

Powered by Blogger.