NEWCASTLE UNITED YATWAA UBINGWA SIKU YA MWISHO KATIKA LIGI YA CHAMPIONSHIP


Kuna msemo unasema "Anayecheka Mwishoni hucheka zaidi" ndivyo ilivyokua kwa klabu kongwe na yenye historia katika ligi ya England Newcastle United wakifanikiwa kuchukua ubingwa katika siku ya mwisho kabisa kwenye kinyang'anyiro cha michuano ya ligi daraja la kwanza England yani Championship.

Newcastle wamefanikiwa kuchukua ubingwa wa michuano hiyo baada ya kuifunga Bansley bao 3-0 huku wapinzani wao wakuu Brighton & Hove Albion wakitoka sare ya bao 1-1 na Aston Villa kwenye mechi za mwisho zilizopigwa zote muda mmoja kuanzia saa 8 kamili kwa saa za hapa nyumbani Tanzania.

Mpaka michezo ya leo inapigwa Newcastle walikua wamezidiwa pointi moja na Brighton huku timu zote hizo zikiwa zimeshapanda daraja na kama Brighton ingeshinda basi ingebeba kombe la ubingwa huo.

Ukiacha Newcastle na Brighton timu zingine nne zitacheza hatua ya mtoano kupata timu moja itakayoungana na Hizo mbili kucheza ligi kuu msimu ujao ambazo ni Reading, Sheffield Wednesday,Huddesfield na Fulham.

Timu zilizoshuka daraja toka katika michuano hiyo ni Wigan,Blackburn na Rotherham United.

No comments

Powered by Blogger.