LIGI YA MABINGWA ULAYA NUSU FAINALI LEO NI MADRID DERBY


Mechi za kwanza katika ligi ya mabingwa Ulaya hatua ya nusu Fainali zinaanza kuchezwa Usiku wa leo barani Ulaya.

Mechi ya leo ni kama marudio ya mechi ya fainali ya michuano hiyo msimu uliopita baina ya Real Madrid ambao ni mabingwa watetezi dhidi ya Atletico Madrid ambao walishika nafasi ya pili.

Msimu huu tayari timu hizo zimeshakutana mara mbili Real Madrid ikishinda moja na sare moja huku mchezo wa leo ukipangwa kuchezwa Santiago Bernabeu nyumbani kwa Real Madrid.

Gareth Bale atakosekana kwa upande wa Real Madrid baada ya kuumia katika mechi ya ElClassico

No comments

Powered by Blogger.