INSIDE UNITED : MAJERUHI WALIOREJEA KIKOSINI WAIPA MATUMAINI MAN UNITED KATIKA EUROPA LEO
Karibu tena leo Alhamisi katika INSIDE UNITED makala ambayo huzungumzia habari za klabu ya Manchester United ambapo leo tunaangalia jinsi gani Kikosi cha kocha Jose Mourinho kitakabiliana na Celta Vigo ya Spain kwenye michuano ya Europa league hatua ya Nusu fainali.
Manchester United imesafiri kwenda Spain ikiwa na ahuweni katika kikosi chake baada ya majeruhi kuanza kurejea kikosini.
Paul Pogba,Juan Mata, Phil Jones,Chriss Smalling na Erick Bailly wote wamerejea kikosini baada ya kukosekana kwa mechi kadhaa kutokana na majeruhi na wachezaji wote hao wamesafiri kwenda Spain kwaajili ya mechi hiyo Muhimu kwa United.
Pambano hilo la leo litaanza majira ya saa 4 kamili Usiku kwa saa za Afrika Mashariki huku mshindi wa jumla katika mechi hii na ile ya marudiano wiki ijayo atapata nafasi ya kucheza fainali mwishoni mwa mwezi huu dhidi ya Ajax au Lyon ambao walicheza jana na Lyon kubugizwa bao 4-1 ugenini.
Kwa leo ni hayo tu tukutane tena kesho ambapo tutaangazia nini kilichotokea Spain na walichosema wachezaji na makocha.
Its me Edo DC

No comments