EUROPA LEAGUE, MAN UNITED YAPATA USHINDI MUHIMU NCHINI SPAIN


Mechi ya pili ya nusu fainali katika michuano ya Europa League baina ya wenyeji Celta Vigo na Manchester United imemalizika kwa United kushinda bao 1-0.

Shujaa wa mchezo huo alikua mshambuliaji Marcus Rashford aliyefunga bao hilo pekee kwa mpira wa adhabu ndogo ambao ulienda moja kwa moja golini na kumshinda kipa wa Celta Vigo.

Timu hizo zitarudiana wiki ijayo ambapo mshindi wa jumla atacheza dhid mshindi wa mechi nyingine ya nusu fainali baina ya Lyon na Ajax huku Ajax wakiwa tayari na faida ya goli 4-1 walizopata katika mechi yao ya jana.


No comments

Powered by Blogger.