EUROPA LEAGUE: AJAX YAIFANYIA KITU MBAYA LYON YAJIWEKA VYEMA KUCHEZA FAINALI


Mechi ya kwanza ya michuano ya Europa League hatua ya nusu fainali imechezwa leo jijini Amstardam baina ya wenyeji Ajax dhidi ya Olympic Lyon ya Ufaransa.

Mechi hiyo imemalizika kwa wenyeji kushinda bao 4-1 ushindi ambao umeifanya Ajax ambayo kikosi chake kinajengwa na vijana wengi kutanguliza mguu mmoja kwenye fainali ya michuano hiyo ya pili kwa ukubwa katika ngazi ya klabu barani Ulaya.

Magoli ya Ajax yalifungwa na Bertrand Traore aliyefunga mabao mawili dakika ya 25 na dakika ya 71, Kasper Dolberg dakika ya 34 na Amin Younes  wakati goli pekee la Lyon lilifungwa na Methieu Valbuena dakika ya 66.

Mechi ya marudiano ni wiki ijayo na mshindi wa jumla atacheza fainali dhidi ya Manchester United au Celta Vigo.

No comments

Powered by Blogger.