EPL : ARSENAL YA KOSAKOSA NAFASI YA LIGI YA MABINGWA ULAYA BAADA YA MIAKA 18,CHELSEA YAKABIDHIWA KOMBE


Miezi 10 ya kinyang'anyiro cha kuwania ubingwa wa soka nchini England ilihitimishwa jana kwa mechi 10 kupigwa kwenye viwanja mbalimbali nchini humo huku historia mpya ikiwekwa baada ya mechi hizo

Mechi mbili baina ya Arsenal na Everton na ile ya Livepool dhidi ya Middlesbrough ndizo zilizovutia zaidi kwani baada ya miaka 18 jana tulishuhudia Arsenal ikishindwa kupata nafasi ya kucheza katika michuano ya ligi ya Mabingwa barani Ulaya baada ya kumaliza ikishindwa kumaliza katika nafasi nne za juu.

Ikiwa nyumbani Arsenal iliibuka na ushindi wa bao 3-1 wakati huo huo Liverpool nao wakaibuka na ushindi wa bao 3-0 Matokeo ambayo yanawafanya Liverpool kuweza kupata nafasi ya kushiriki michuano ya ligi ya Mabingwa barani Ulaya huku Arsenal ikitakiwa sasa kushiriki katika michuano ya Europa League msimu ujao ikiwa ni miaka 18 tangu Arsenal iliposhindwa kushiriki katika michuano hiyo.

Chelsea wao wakiwa nyumbani waliweza kuifunga Sunderland bao 5-1  katika mechi ambayo Chelsea ilikabidhiwa ubingwa wa msimu huu ikiwa ni ubingwa wao wa 6 katika historia ya klabu hiyo.

Manchester United wao wakiwa nyumbani jana ilishuhudiwa kwa mara ya kwanza katika historia wakichezesha kikosi kilichojaa vijana wengi na kuweza kuibuka na ushindi wa bao 2-0.

Tottenham wao ndiyo waliovunja rekodi jana wakiibuka na ushindi wa bao 7-1 katika mechi ambayo Harry Kane alifunga Hat-trick na kumfanya kuwa mfungaji bora wa msimu huu akifikisha magoli 29.

Mpaka mwisho wa ligi jana Chelsea Ndio waliobahatika kupata ubingwa wakiwa na pointi 93 wakifatiwa na Tottenham waliokua na pointi 86 huku Manchester City wao wakishika nafasi ya 3 wakiwa na pointi 78,Liverpool wao wakishika nafasi ya 4 wakiwa na pointi 76 na Arsenal wakiwa na pointi 75 katika nafasi ya 5.

Hull City, Sunderland na Middlesbrough ndizo zilizoshuka daraja kutoka katika ligi hiyo.

No comments

Powered by Blogger.