SIMBA YAIBUKA NA USHINDI WA MAAJABU MWANZA
Wekundu wa Msimbazi Simba wameibuka na ushindi unaoweza kuuita ni wa maajabu baada ya kuwalaza Mbao FC bao 3-2.
Mchezo huo wa ligi kuu Tanzania bara kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ulitawaliwa zaidi na vijana wa Mbao FC kipindi cha kwanza huku Simba wao wakitawala kipindi cha pili.
Simba ilipata mabao mawili ya kusawazisha kupitia kwa mshambuliaji wake raia wa Ivory Coast Fredric Blagnon ambaye aliingia katika mchezo huo akitokea benchi kuchukua nafasi ya Juma Luizio ikiwa ni mchezo wake wa kwanza katika ligi baada ya jaribio lake la kutaka kuihama klabu hiyo kushindikana huku Mzamiru Yasin akiibuka shujaa wa mchezo huo akifunga bao la ushindi dakika ya mwisho katika muda wa nyongeza.
Kwa matokeo hayo Simba sasa wanafikisha pointi 58 na kurudi kileleni mwa msimamo wa ligi kuu soka Tanzania bara huku Mahasimu wao Yanga wakibaki na pointi 56 katika nafasi ya pili.

No comments