ARSENAL NDO KAMA ULIVYOSIKIA, YAKUBALI KICHAPO CHA NGUVU EPL
Hali imeendelea kuwa tete kwa kocha Arsene Wenger baada ya kukubali kufungwa bao 3-0 na Crystal Palace katika mechi ya ligi kuu ya England.
Arsenal walioingia katika mchezo huo wakiwa na matumaini ya kupata ushindi na kuondoka katika nafasi ya 6 waliyonayo hivi sasa ilijikuta ikipata kipigo hicho wakiwa ugenini.
Andros Townsend mchezaji wa zamani wa Tottenham na Newcastle ndiye aliyefungua ukurasa wa mabao kwa Crystal palace baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Wilfried Zaha dakika ya 17 ya mchezo bao lililodumu mpaka mapumziko.
Kipindi cha pili mambo yaliendelea kuwa magumu kwa Arsenal kwani dakika ya 63 kiungo wa zamani wa Newcastle United na PSG Yohan Kabaye aliipatia Palace bao la pili wakati Luka Milivojevic akifunga bao la tatu kwa njia ya penati.
No comments