NEWCASTLE KUREJEA LIGI KUU ENGLAND LEO?


Mwaka Mmoja katika ligi daraja la kwanza nchini England maarufu kama Championship unaweza kukamilika leo na kushuhudia vigogo wa zamani katika soka la England klabu ya Newcastle United huenda ikarejea tena kwenye ligi kuu ya Englan leo usiku.

Newcastle United imebakiza mechi 3 na ikihitaji pointi 3 tu katika mechi hizo ili kujihakikishia kupanda daraja huku ikiendelea pia kujaribu kushinda ubingwa.

Tiketi ya Newcastle United leo imeshikwa na Preston North End ambao watacheza nao usiku huu kwenye dimba la St. James Park.

Kocha Rafael Benitez ambaye alikubali kushuka daraja na timu hiyo na kusaini mkataba wa miaka mitatu alipewa majukumu matatu la kwanza lilikua kuipandisha daraja Newcastle la pili ni kuiweka katika ligi kuu na la tatu kuirudisha timu katika michuano ya Ulaya.

Kama Newcastle itashinda leo itafikisha pointi 88 na kuungana na Brighton ambao tayari wameshakata tiketi ya kupanda daraja wenye pointi 92 wanaoongoza ligi hiyo.

No comments

Powered by Blogger.