MONACO YATINGA NUSU FAINALI KIBABE MABINGWA BARANI ULAYA.
Vinara wa ligi kuu ya Ufaransa klabu ya Monaco jana iliendeleza msimu mzuri kwa klabu hiyo wakitinga hatua ya nusu fainali katika hatua ya ligi ya mabingwa barani Ulaya wakiitupa nje ya michuano hiyo Borussia Dortmund ya Ujerumani.
Ikiwa nyumbani jana Monaco iliweza kuibuka na ushindi wa bao 3-1 ikiwa ni mechi ya marudiano baada ya ile ya awali ambayo Monaco walishinda pia bao 3-2 ugenini hivyo kufanikiwa kutinga nusu fainali kwa ushindi wa jumla wa bao 6-3.
Chipukizi Kylian Mbappe Lotin alifungua ukurasa wa mabao kwa Monaco dakika ya 3 tu kisha Nahodha Radamel Falcao akafunga bao la pili dakika 9 baadae na kufanya mchezo huo kwenda mapumziko Monaco wakiwa tayari mbele kwa bao hizo 2-0.
Kipindi cha pili Borussia Dortmund waliweza kuzinduka na kupata bao la kufutia machozi likifungwa na Marco Reus dakika ya 48 ambalo lilifufua matumaini kwa Dortmund lakini wakashindwa kupata mabao mengine na kuruhusu Monaco kupata bao la tatu dakika ya 81 likifungwa na Valere Germain.
Monaco wanaungana na Real Madrid, Juventus na Atletico Madrid kucheza hatua ya nusu fainali.

No comments