LA LIGA JANA : REAL MARID SARE BARCELONA YACHAPWA,SEVILLA MAMBO SAFI
Mabingwa watetezi wa ligi kuu nchini Spain klabu ya Barcelona jana ilijikuta ikipoteza mchezo muhimu ambao ungeiweka kileleni mwa maimamo wa ligi hiyo inayokaribia kumalizika.
Barcelona ikicheza ugenini katika mechi ya mwisho katika ligi hiyo jana Jumamosi ilijikuta ikifungwa bao 2-0 na wenyeji Malaga katika mchezo ambao mshambuliaji wa Barcelona Neymar alitolewa kwa kadi nyekundu.
Awali katika mchezo ambao wengi waliona ni nafasi kwa Barcelona kurudi kileleni Real Madrid walitoka sare ya bao 1-1 na Wageni Atletico Madrid Pepe akitangulia kufunga kabla ya Antoine Griezman hajaisawazishia Atletico Madrid.
Espanyol yenyewe iliweza kuinyuka Alaves bao 1-0 katika mchezo wa mapema kabisa bao pekee likifungwa na Pablo Piatti.
Sevilla baada ya matokeo mabaya katika mechi zake za hivi karibuni jana walirudisha furaha ya ushindi wakiifunga Deportivo la Coruna bao 4-2.
Kwa matokeo ya jana Real Madrid wanaendelea kuongoza wakiwa na pointi zao 72 huku wakiwa na mchezo mmoja mkononi wakifatiwa na Barcelona wenye pointi 69.
No comments