KLABU NYINGINE MAREKANI YATANGAZA KUMWANIA IBRAHIMOVIC

Los Angeles FC klabu mpya iliyopanda kucheza ligi kuu nchini Marekani MLS imetangaza nia ya kumwania mshambuliaji mkongwe wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic.

LA FC inaungana na LA Galaxy ambao nao walishaonesha nia ya kumwania nguli huyo wa zamani wa Sweden.

Tayari timu hiyo imeweka mezani kiasi cha paundi 260,000 kumwania nyota huyo ambaye mkataba wake na Manchester United utamalizika mwishoni mwa msimu huu huku wakitangaza kuwa tayari kumruhusu mchezaji huyo kuichezea Manchester United kwenye michuano ya Ulaya kwa mkopo.

Bado haijafahamika kwamba Manchester United watamwachia mchezaji huyo na inasemekana mazungumzo yanaendelea kuweza kumbakiza Old Trafford.

UNADHANI MAN UNITED WANAPASWA KUMWACHIA ZLATAN? TOA MAONI YAKO HAPA.

No comments

Powered by Blogger.