INSIDE UNITED : MAN UNITED YAPOTEZA NAFASI YA KUINGIA TOP 4 KWA SARE NYUMBANI


Leo katika INSIDE UNITED tunaangalia kilichotokea katika mchezo dhidi ya Swansea City ambao ulifanyika katika dimba la Old Trafford na kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Huu ni mchezo ambao sio tu umeyumbisha nafasi ya kuingia Top 4 Lakini pia umezidisha majeruhi katika kikosi kuelekea katika mechi muhimu za mwisho wa msimu.

Eric Bailly na Luke Shaw wote walitolewa katika mechi ya leo baada ya kuumia na kuongeza mlolongo wa majeruhi kikosini wakiungana na Jones,Smalling,Rojo,Pogba na Zlatan Ibrahimovic.

Habari njema kwa United leo ni kurejea kwa Juan Mata ambaye alikua katika benchi leo licha ya taarifa za awali kusema angerejea Alhamis katika mechi dhidi ya Celta Vigo.

Paul Pogba nae anaendelea vizuri na huenda akarejea dimbani katika mechi ijayo lakini hali inazidi kuwa ngumu katika upande wa beki wa kati baada ya mabeki wote sasa kuwa majeruhi.

Habari njema kwa United pia ni Manchester City kutoka sare na Middlesbrough wakati Arsenal wamepoteza dhidi ya Tottenham hivyo mchakato wa kuwania Top 4 ukibaki kama ulivyo na laiti kama tungeshinda leo basi tungepaa mpaka nafasi ya 3.

Ni hayo tu kwa leo tukutane kesho kuangalia nini kimetokea katika Manchester United.


No comments

Powered by Blogger.