CHELSEA YAENDELEA KUPAA KILELENI EPL


Vinara wa ligi kuu ya Soka nchini England klabu ya Chelsea jana Usiku ilihakikisha inajiimarisha kileleni baada ya kuibuka na ushindi wa bao 4-2.

Mechi hiyo iliyochezwa Darajani ilikua dhidi ya Southampton,mechi ambayo haikuwa rahisi kwa Chelsea baada ya Southampton kuonyesha kiwango cha hali ya juu japo makosa machache ndiyo yaliyoimaliza.

Eden Hazard, alitangulia kuifungia Chelsea bao la kwanza kabla ya Oriol Romeu ambaye alishawahi kuichezea Chelsea hajaisawazishia Southampton lakini Gary Cahill aliipatia Chelsea bao la pili dakika moja kabla ya mapumziko.

Diego Costa akafunga bao 2 zaidi kipindi cha pili kuihakikishia Chelsea ushindi huku Ryan Bertrand akifunga bao la pili kwa Southampton.

No comments

Powered by Blogger.