BAADA YA MIAKA 34 BRIGHTON YAREJEA LIGI KUU YA ENGLAND
Moja kati ya ligi zenye ushindani mkubwa na pesa nyingi duniani ni ligi kuu ya England na timu kupanda mpaka kucheza katika ligi hiyo huwa ni ngumu sana kutokana na ushindani uliopo katika ligi daraja la kwanza maarufu kama Championship.
Ndani ya miaka 34 klabu ya Brighton & Hove Albion ikipigania kupanda daraja hatimaye timu hiyo imepata nafasi ya kupanda daraja kucheza ligi kuu msimu ujao.
Brighton jana waliibuka na ushindi wa bao 2-1 nyumbani dhidi ya Wigan Athletic katika mchezo ambao umeifanya Brighton kurejea katika ligi kuu kwa mara ya kwanza tangu iliposhuka msimu wa mwaka 1982/1983.
Brighton imefikisha pointi 92 ikiwa ni kinara wa ligi hiyo na kupata moja kati ya timu 3 zitakazopanda daraja msimu ujao huku ikihitaji pointi 3 tu kuweza kutwaa ubingwa wa michuano hiyo.
Msafara wa ubingwa wa michuano hiyo ulikua ukitawaliwa na timu mbili Brighton na Newcastle United ambao katika siku za hivi karibuni Newcastle wamepoteza pumzi ya kuendelea kushindania ubingwa ikiwa katika nafasi ya pili wakiwa na pointi 85.
Timu mbili za Juu katika msimamo wa ligi daraja la kwanza hupanda mara moja katika ligi kuu huku timu ya tatu mpaka timu ya 6 zikicheza hatua ya mtoano.

No comments