BAADA YA MIAKA 22 CHELSEA, JOHN TERRY ATANGAZA KUIHAMA KLABU HIYO
Miaka 22 ya kuitumikia Chelsea inaelekea ukingoni mwishoni mwa msimu huu kwa nahodha wa klabu hiyo John Terry baada ya kutangaza kuihama mwishoni mwa msimu huu.
John Terry kupitia ukurasa wake wa Instagram jana Jumatatu alitangaza nia yake ya kuondoka ndani ya Chelsea lakini amesisitiza kwamba bado hafikirii kustaafu soka na kwa maana hiyo atatafuta klabu nyingine ya kuichezea msimu ujao.
Chelsea alipanga kuihama klabu hiyo mapema mwanzoni mwa msimu huu lakini nia ya kocha wa Chelsea kumbakiza kikosini kulimpa nia ya kuendelea kuitumikia japo sasa anaona hapati tena muda wa kucheza hivyo kumlazimu kuondoka.
Miaka 22 katika klabu hiyo imempa mafanikio makubwa kwake kwani ameweza kucheza mechi 713 na kufanikiwa kufunga magoli 66 na kuwa ndiye mchezaji wa kwanza katika ligi kuu ya England anayeongoza kwa kufunga mabao mengi akicheza katika nafasi ya Ulinzi.
Amefanikiwa kushinda makombe 14 manne ya ligi kuu ya England, moja katika ligi ya mabingwa Ulaya, moja pia katika michuano ya Europa League na matatu katika kombe la ligi nchini England na matano ya kombe la FA.
Stoke City,Bournemouth na West Brom zote zilionyesha nia ya kumsajili mchezaji huyo mwezi January mwaka huu.
Best Epl defender of all time
ReplyDelete