ALICHOSEMA WAZIRI MWAKYEMBE KUHUSU SOKA LA BONGO
Waziri wa Habari,utamaduni sanaa na michezo Dr Harrison Mwakyembe amewaomba watanzania wajitokeze kwa wingi katika kuhakikisha wanasaidia timu ya soka ya Serengeti boys.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na www.wapendasoka.com akiwa katika ziara wilayani Kwimba jijini Mwanza, Dr. Mwakyembe alisema watanzania waiunge mkono Serengeti boys ili Iweze kucheza kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana nchini Gabon baada ya hapo waweze kufuzu kwajili ya kucheza kombe la Dunia la vijana nchini India mwezi wa 11 mwaka huu.
Mheshimwa Dr. Mwakyembe alisema ana imani kubwa na timu hiyo kuwa itafanya vyema na ameahidi kuendelea kuisapoti.
Aidha Waziri Mwakyembe ameipongeza pia timu ya taifa 'Taifa stars" kwa matokeo mazuri waliyopata dhidi ya Botswana na Burundi hivi karibuni.
Waziri Mwakyembe ameziomba sekta binafsi kuhakikisha zinachangia katika kuinua elimu ya michezo.Pia waziri huyo alisema kamati ya ufundi zimedidimiza sana soka nchini kutokana na mambo yao ya kuamini sana katika mambo ya ushirikiana kuliko kufanya mazoezi.

No comments