YANGA YAANGUKIA MIKONONI MWA WAARABU
Yanga imepangwa kucheza dhidi ya Mouloudia Club d'Alger, maarufu kama MC Alger
ya Algeria katika mchujo wa kuwania hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho
Afrika baada ya droo iliyopangwa mchana huu mjini Cairo, Misri yalipo makao
makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
Droo hiyo imehusisha timu zilizovuka hatua ya 32
Bora ya Kombe la Shirikisho dhidi ya zilizotolewa kwenye hatua hiyo ya Ligi ya
Mabingwa Afrika.
Timu zilizotolewa Ligi ya Mabingwa zitamenyana na
zilizosonga mbele Kombe la Shirikisho katika mechi za nyumbani na ugenini
kuwania nafasi ya kucheza hatua ya makundi ya michuano hiyo ya pili kwa ukubwa
kwa ngazi ya klabu barani Afrika.
Mechi za kwanza zinatarajiwa kucheza wikiendi ya
Aprili 7 hadi 9 na marudiano yanatarajiwa kuwa wikiendi ya Aprili 14 hadi 16,
mwaka huu.
Yanga
imeangukia Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kutolewa katika michuano
ya Ligi ya Mabingwa baada ya sare ya 0-0 na wenyeji, Zanacio Jumamosi Uwanja wa
Taifa wa Mashujaa, Lusaka nchini Zambia.
Matokeo hayo yanamaanisha Yanga imetolewa kwa mabao
ya ugenini, baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza wiki
iliyopita Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

No comments