MAYANGA ATEUA MANAHODHA

Kocha Mkuu wa timu wa Taifa, Salum Mayanga amemteuwa Himid Mao na Jonas Mkude kuwa manahodha wasaidizi huku akimuwenguo cheo hicho John Bocco.


Akizungumza na.... Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas alisema baada ya kufanya mabadiliko ya benchi la ufundi, halitafanya mabadiliko kwa nahodha mkuu ambaye ataendelea kubaki na Mbwana Samatta.

Alisema mabadiliko hayo yatafanyika kwa wasaidizi hao baada ya kutoitwa na Bocco katika kikosi cha timu.

"Mabadiliko hayo yamefanyika kwa wasaidizi pekee, hivyo Samatta ataendelea na majukumu yake katika mechi za Fifa ambapo michuano ya CHAN yakisimamiwa na Himid pamoja ma Mkude," alisema Alfred.


Alisema Samatta anatarajia kuingia leo saa 4 usiku na Farid Mussa akiingia saa 10 Alfajir na kesho kwenda kupimwa Afya zao ikiwemo mapigo ya moyo kabla kuwavaa wapinzani wao Bostwana jumamosi uwanja wa Taifa.

No comments

Powered by Blogger.