STARS NI MWENDO WA KUGAWA DOZI TU, BURUNDI YA MAVUGO HOI TAIFA
Nyota njema inaendelea kuiwakia Taifa Stars chini ya kocha Mzalendo Jackson Mayanga baada ya leo kuikandamiza Burundi bao 2-1.
Mchezo huo wa kimataifa wa kirafiki ulichezwa katika dimba la Taifa Jijini Dar es Salaam ambapo ni wa pili kwa kikosi kipya cha timu ya Taifa chini ya Mayanja.
Kinara wa kupachika mabao katika ligi kuu Tanzania bara Simon Msuva alitangulia kuipatia Taifa Stars bao la kwanza bao ambalo lilidumu mpaka mapumziko.
Kipindi cha pili Burundi walizinduka na kusawazisha bao hilo likifungwa na Mshambuliaji wa timu hiyo anayeichezea Simba SC Laudit Mavugo baada ya mabeki kuchanganyana na mkali huyo wa kupachika mabao kufunga kirahisi.
Mshambuliaji mpya wa Taifa Stars Mbaraka Yusuph ambaye huichezea pia Kagera Sugar ya mkoani Kagera ndiye aliyerudisha tabasamu katika nyuso za Watanzania akifunga bao la ushindi kwa Taifa Stars zikiwa zimebaki dakika chache kabla ya mpira kuisha.
Taifa Stars leo ilicheza bila ya nahodha wake Mbwana Samata ambaye ameshaondoka nchini kurudi Ubelgiji kwaajili ya mechi ya ligi ya huko wikiend hii akiwa na klabu yake ya Genk.
Ushindi huu umekuja siku chache baada ya kuwafunga Botswana katika mechi iliyochezwa Jumamosi.

No comments