SAMATTA AONYESHA MAMBO YA ULAYA, TAIFA STARS IKIIANGAMIZA BOTSWANA


Nahodha wa timu ya Taifa Ya Tanzania na mshambuliaji wa KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Ally Samatta amefunga mabao yote mawili ya Taifa Stars dhidi ya Botswana.

Mchezo huo wa kimataifa wa Kirafiki ulipigwa katika dimba la Taifa Jijini na Taifa Stars kuibuka na ushindi wa bao 2-0.

Mchezo huo ambao ni wa kwanza kwa kocha Jackson Mayanja ambaye ameteuliwa rasmi kuiongoza Taifa Stars baada ya kuondoka kwa Charles Mkwasa.

Iimchukua dakika 2 tu Samata kupata bao la kwanza akipokea pasi ya Mohamed Hussein Zimbwe na kuwakimbia walinzi wa Botswana wakidhani angetoa pasi lakini akafumua shuti kali lililojaa wavuni goli ambalo lilidumu mpaka mapumziko.

Kupindi cha pili Botswana walibadilika na kutandaza soka safi huku wakiliandama lango la Stars lakini uhodari wa Samata ulifanikiwa kuipatia Stars bao la pili kwa njia ya adhabu ndogo dakika ya 87 baada ya kufanyiwa faulo iliyozaa goli.

Taifa Stars itacheza na Burundi katika mechi nyingine ya kujipima nguvu Jumanne wiki hii.

No comments

Powered by Blogger.