KAMA WENGER ASIPOONDOKA, ARSENAL ISAHAU KUHUSU KIPA SZCZESNY

Kipa Raia wa Poland Wojciech Szczesny anayeichezea AS Roma kwa mkopo akitokea Arsenal atalazimisha kubaki kwenye klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya Italia Serie A kama Kocha Arsene Wenger atapewa mkataba mpya na kubaki Arsenal.

Rais wa shirikisho la soka nchini Poland Zbigniew Boniak amesema kipa huyo namba moja wa Poland amemwelezea kipa huyo kwamba alimweleza hafikirii kurejea Arsenal baada ya mkopo wake kuisha na angependa zaidi na AS Roma ambayo imeonekana kumthamini.

Kocha Arsene Wenger ambaye ndiye   aliyempeleka kipa huyo Roma kwa mkopo wa miaka miwili ambao utamalizika  mwishoni mwa msimu huu wakati mkataba wake na Arsenal utamalizika mwaka 2019 amekalia kuti kavu baada ya shinikizo kubwa kutoka kwa  mashabiki wakitaka aondolewe katika timu hiyo lakini kuna uwezekano pia akapewa mkataba mpya wa miaka miwili unaozungumzwa.

No comments

Powered by Blogger.