MCHEZO WA MBAO FC NA SIMBA WASOGEZWA MBELE

Shirikisho la Soka Nchini Tanzania TFF kupitia bodi ya ligi Tanzania bara limesogeza mbele mchezo wa ligi kuu ya soka  Tanzania bara kati ya Mbao FC na Vinara wa ligi hiyo Simba SC.

Awali mchezo huo ulipangwa kufanyika tarehe 8/04/2017 lakini kutokana a mabadiliko hayo sasa mchezo huo utapigwa siku mbili baadae yani tarehe 10/04/2017 katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.

Imeelezwa sababu kuu za kupigwa kalenda mchezo huo ni uwanja wa CCM Kirumba kuwa katika shughuli nyingine ambazo zitaanza tarehe 1/04/2017 mpaka tarehe 9/04/2017.

Ligi kuu imesimama hivi sasa kupisha michezo ya kimataifa ambapo mpaka inasimama Simba ndiyo wanaoongoza ligi hiyo wakiwa na pointi 55 wakati Mbao FC wao wanashika nafasi ya 11 wakiwa na pointi 27.

No comments

Powered by Blogger.