MAN UNITED YATENGA PESA YA KUFURU KUMSAJILI NEYMAR TOKA BARCELONA
Gazeti la michezo la Sport la Spain limeripot leo kwamba Manchester United imetenga kiasi cha Euro milioni 200 sawa na paundi milioni 173 kumsajili nyota wa kimataifa wa Brazil na klabu ya Barcelona Neymar.
Wiki iliyopita Neymar alisema angetamani siku moja kufanya kazi England huku akivitaja vilabu kama Manchester United,Arsenal na Liverpool kati ya vilabu vinavyosifika na vyenye mashabiki wengi duniani.
Huku akiwataja Jose Mourinho na Pep Guadiola kuwa ni makocha wa kiwango cha juu ambao kila mchezaji angependa kufanya kazi nao.
Sambamba na pesa hizo nyingi ambazo Barcelona watapata na kuvunja kabisa usajili uliowahi kufanywa wa fedha nyingi lakini pia Neymar atakua mchezaji wa kwanza kulipwa fedha nyingi zaidi duniani akilipwa paundi 416,000 kwa wiki.
Bado haijafahamika zaidi kama kweli kiwango hiki ndicho kilichowekwa na United huku kukiwa hakuna uthibitisho toka katika vilabu vyote viwili.

No comments