HATIMAYE MAN UNITED YAWAACHIA ARSENAL NAFASI YA 6 EPL
Baada ya kusota kwa muda mrefu katika nafasi ya 6 hatimaye Manchester United imeondoka katika nafasi hiyo kwa ushindi wa bao 3-1 walioupata mchana wa leo dhidi ya Middlesbrough.
Maroane Fellaini alitangulia kuifungia Manchester United bao la kwanza dakika ya 30 bao ambalo lilidumu mpaka mapumziko.
Kipindi cha pili United waliongeza mashambulizi na kufanikiwa kupata bao la pili dakika ya 65 likifungwa na Jesse Lingard kwa shuti kali nje ya 18.
Gestede wa Middlesbrough aliipatia bao la kufutia machozi dakika ya 77 kabla ya Valencia hajafunga bao la 3 kwa United baada ya makosa ya Kipa Victor Valdes aliyeteleza na kumwacha mfungaji akibaki yeye na goli.
Kwa matokeo hayo Man United inafikisha pointi 52 pointi 2 mbele ya Arsenal ambao sasa wanashika nafasi ya 6.

No comments