FALCAO AUMIA MONACO IKIPATA USHINDI MUHIMU LIGI KUU UFARANSA


Nahodha wa Monaco Radamel Falcao jana alitolewa uwanjani baada ya kuumia nyonga wakati Monaco wakiibuka na ushindi muhimu wa bao 2-1 dhidi ya Boudeux kwenye ligi kuu ya Ufaransa.

Ikicheza nyumbani Monaco ambao ni vinara wa ligi hiyo walijikuta wakimpoteza nahodha wao huyo zikiwa zimebaki siku chache kabla hawajaikabili Manchester City katika mechi ya klabu bingwa Ulaya wiki hii.

Joao Mortinho na Kyllan Mbappe Lottin waliifungia Monaco hiyo jana ambayo inahangaika kusaka ubingwa wa Ufaransa tangu walipofanya hivyo mwaka 2000.

Katika mechi zingine hiyo jana Guingamp iliifunga Bastia bao 5-0, Montepellier ikafungwa 3-2 nyumbani na Nantes,Lille ikaibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Nancy wakati Rennes na Dijon zikitoka sare ya bao 1-1.

No comments

Powered by Blogger.