BUNDESLIGA JANA: BAYERN MUNICH YAJISAFISHIA NJIA YA UBINGWA, DORTMUND NA RB LEIPZIG ZACHAPWA


Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga, Bayern Munich wameongeza wigo wa pointi dhidi ya anayeshika nafasi ya pili kufikia 10 katika harakati za kutetea ubingwa wao.

Wakiwa nyumbani jana siku chache baada ya kuibuka na ushindi mkubwa kwenye ligi ya mabingwa Ulaya,Bayern waliibuka na ushindi wa bao  3-0 dhidi ya Eintracht Frankfurt mabao mawili ya Lewandowski na moja la Douglas Costa.

Katika mechi zingine hiyo jana timu ngeni ya RB Leipzig licha ya kuendelea kushika nafasi ya pili ilijikuta ikipoteza mchezo wake wa jana tena ikiwa nyumbani dhidi ya Wolfsburg wakati wapinzani wakuu wa Bayern Munich Borussia Dortmund wao wakipoteza mechi yao dhidi ya Hertha Berlin kwa kufungwa bao 2-1 ugenini.

MATOKEO YA MECHI ZOTE ZA JANA BUNDESLIGA


  • Bayern Munich 3-0 Frankfurt
  • RB Leipzig 0-1 Wolfsburg
  • Hertha Berlin 2-1 Dortmund
  • Damstadt 2-1 Mainz 05
  • Ingolstadt 2-2 FC Cologne
  • Freiburg 1-1 Hoffenheim

No comments

Powered by Blogger.