BAADA YA KUTOLEWA KOMBE LA SHIRIKISHO, AZAM FC WALIA NA HUJUMA.

Weekend Imeisha vibaya kwa wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kimataifa baada ya Azam Fc na Yanga kutolewa katika michuano ya kombe la shirikisho na klabu bingwa Afrika wote wakicheza ugenini.

Tofauti na Yanga ambao licha ya kutolewa katika michuano ya klabu bingwa Afrika watacheza mechi moja katika michuano ya kombe la Shirikisho ili kukata tiketi ya kucheza makundi, Azam Fc wao wametolewa mazima katika michuano hiyo ya kombe la shirikisho baada ya kutupwa nje kwa kufungwa jumla ya mabao 3-1.

 Uongozi wa timu hiyo yenye makazi yake Chamazi jijini Dar es Salaam wamelia na hujuma walizofanyiwa kwenye mchezo wao wa marudiano dhidi ya Mbabane Swallows ya Swaziland.

Inasemekana vyumba vya kubadilishia nguo wachezaji vilipuliziwa dawa ambayo haikua sahihi kwa matumizi ya binadamu ambayo ilikua na lengo la kuwadhoofisha pia kuwaondoa mchezoni wachezaji wao.

Azam FC katika mchezo huo wa jana walifungwa bao 3-0 licha ya ushindi wa bao 1-0 walioupata Dar es Salaam wiki iliyopita.

Azam Sasa wanarejea nyumbani kujaribu kupata tena nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa kwa kushinda ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara ubingwa ambao hauonekani kuwa halisia kwao kushinda baada ya kuachwa pointi nyingi na Simba na Yanga lakini kwenye kombe la FA wana kibarua cha kawaida kuweza kufuzu nusu fainali watakapocheza dhdi ya Ndanda FC ya Mtwara.





No comments

Powered by Blogger.