BAADA YA KIPIGO KUTOKA KWA WATANI ZAO YANGA YAOMBA RADHI
Young Africans Sports Club kupitia katibu mkuu wake
Boniface Charles Mkwasa, inawaomba radhi wanachama wote, wapenzi na mashabiki
wa klabu yetu pendwa Young Africans kwa matokeo ya Jumamosi dhidi ya Simba SC
kwa kupoteza 2-1.
Klabu inawaomba kuwa watulivu na pia inashukuru sana
kwa utulivu mliouonyesha na kutii sheria zote kwenye mchezo wa Jumamosi.
Matokeo haya tuliopata ni ya kimchezo kikubwa ni
kupambana na michezo iliyobaki mbele yetu na kuendelea kuwapa sapoti vijana
wetu kwani bado tuna mashindano mengi na michezo mingi mbeleni.
Tunaamini Mwalimu ameona mapungufu kwenye mchezo
uliopita na atayafanyia kazi kuelekea michezo ijayo na tutafanya vizuri na
kurejesha furaha yetu.
Uongozi unaamini wanachama na wapenzi wa Yanga wataendeleza
utulivu na kuendelea kuipa sapoti timu yao kama ilivyo jadi yao.
DAIMA MBELE NYUMA MWIKO.
Imetolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano.
Young African Sports Club.

No comments