YANGA YABEBA POINTI ZOTE 3 KWA MAJIMAJI SONGEA
Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka Tanzania bara Yanga imefanikiwa kuzoa pointi zote 3 katika mchezo wake wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Majimaji FC.
Mchezo huo wa ligi kuu Umemalizika muda mfupi uliopita katika uwanja wa Majimaji Mjini Songea na Yanga kuibuka wababe kwa ushindi mwembamba wa bao 1-0.
Goli pekee la Yanga katika mchezo huo lilifungwa na Deus Kaseka ushindi ambao unawafanya Yanga kufikisha pointi 43 katika nafasi ya pili ikiwa ni pointi 1 nyuma ya Simba wanaoongoza ligi hiyo.
No comments