WAPENDA SOKA DAY YAFANYIKA KWA MAFANIKIO MAKUBWA DAR


Tarehe 1 Januari kila mwaka taasisi ya WAPENDA SOKA TANZANIA imeitenga kuwa siku maalumu ya kusaidia watu wenye mahitaji hasa watoto yatima.

Ni mwaka wa 5 Shughuli hii imefanyika katika jiji la Dar es Salaam pamoja na mjini Bagamoyo lengo kuu likiwa kurudisha shukrani zetu kwa Mungu na jamii kwa kumaliza mwaka salama na kuomba baraka zake kwa mwaka mpya.

Mwaka 2017 Wapenda Soka Tulipata wasaa wa kutembelea makazi ya watoto Yatima HIDAYA yaliyoko CHANIKA ZINGIZIWA nje kidogo ya jijo la Dar es Salaam.

Pamoja na kukabidhi vifaa mbalimbali lakini Wanachama walipata fursa ya kupika vyakula kula na kufurahi pamoja na watoto.
Kushoto ni C.E.O wa Wapenda Soka Tanzania
Pamoja na misaada hiyo michache lakini bado kituo hicho kina changamoto nyingi kwani bado majengo ya kituo hicho hayajakamilika,uhaba wa vitanda na magodoro,vyandarua na umeme.

Tunawaomba watu wote watakaoguswa wasisite kuwasiliana nasi tusaidiane kutatua changamoto hizo unaweza kutupata kwa namba 0653 229 559.

BAADHI YA PICHA ZA MATUKIO



















No comments

Powered by Blogger.