WAKATI BARCELONA IKITOKA SARE NA BETIS,REAL MADRID YAIKANDAMIZA SOCIEDAD NA KUJIIMARISHA KILELENI

Ligi kuu ya Spain imeendelea kushika kasi kwa miamba ya ligi hiyo kuendelea kukimbizana katika kuwania ubingwa msimu huu.



Barcelona ikisafiri kuwakabili Real Betis inayokamata nafasi ya 13 kwenye msimamo ilijikuta ikiambulia sare ya bao 1-1 huku mabao mawili yakikataliwa japo picha za video zinaonyesha mpira ulishavuka mstari wa goli.

Alexandre Alegri alitangulia kuipatia Real Betis bao kabla ya Luis Suarez hajaisawazishia Barcelona huku kukiwa tayari umekataliwa mabao mawili mwamuzi akiwa hajaona mpira ukivuka mstari wa goli.

Real Madrid wao kwa upande wao wakiwa Nyumbani waliweza kuifunga Real Sociedad bao 3-0 magoli ya Mateo Kovavic,Cristiano Ronaldo na Alvaro Morata.

Ushindi huo unawapa mwanya Real Madrid kuendelea kuongeza wigo wa pointi kileleni ikifikisha jumla ya pointi 46 ikiwa na mchezo mmoja mkononi wakati Barcelona wao wana pointi 42 katika nafasi ya pii sawa na Sevilla.

MATOKEO YOTE YA LALIGA JANA


  • Real Betis 1-1 Barcelona
  • Espanyol 3-1 Sevilla
  • Athletic Bilbao 2-1 Sporting Gijon
  • Real Madrid 3-0 Real Sociedad

No comments

Powered by Blogger.