AFCON 2017 : GHANA NA MISRI ZATINGA NUSU FAINALI
Hatua ya pili ya mechi za Robo fainali za michuano ya kombe la mataifa ya Afrika AFCON 2017 zilichezwa jana usiku na kushuhudia Misri na Ghana zikitinga hatua ya nusu fainali.
Katika mechi ya awali jana Ghana iliweza kuifunga Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) bao 2-1 shukrani ziwaendee watoto wa gwiji wa zamani wa Ghana Jordan Ayew aliyefunga bao la kwanza na nduguye Andre Ayew aliyefunga bao la pili huku bao pekee la Congo likifungwa na Paul-Jose M'Poku.
Mechi ya mwisho jana ilizikutanisha timu za Misri na Morocco ambapo mpaka dakika 90 zinamalizika ni Misri ndiyo walioibuka wababe kwa kushinda bao 1-0 bao pekee la dakika ya 88 la Mahmoud Kahraba.
Misri sasa itacheza na Bukina Faso wakati Ghana watacheza dhidi ya Cameroon katika hatua ya Nusu fainali mechi zitakazaaochezwa siku ya Jumatano na Alhamisi saa 4 kamili usiku.

No comments